Kwa kuanza napenda kumshukuru Mungu mola wa viumbe wote, ama baada ya shukurani kwa Mola alie umba mbingu na ardhi na vilivyomo vyote napenda kuelezea Jimbo la Gando.
Gando ni Jimbo ambalo linapatikana katika mkoa wa kaskazini,Wilaya ya Wete Pemba,wakaazi wa Gando ni takribani watu 4000,asilimia 99% ni wafuasi wa dini ya kiislamu, watu wa kijiji cha Gando wengi wao nimaskini wasio jiweza kumiliki mahitaji yao ya msingi ya kila siku, ingawaje Gando imebarikiwa ardhi yenye rutuba pamoja na uzalishaji wamazao ya kuuza, na vipaji vingi vinavochipukia kiutaalamu wa kielimu, bahati mbaya utaalamu huo unafifia mapema bila kufikia malengo na uzalishaji haukidhi haja nakupelekea kila siku zikienda mbele hali ya kiuchumi inazidi kua mbaya kutokana na uhaba wa mambo tofauti katika eneo hili.
Gando ina idadi ya shule saba;-
1.SHULE YA SEKONDARI YA GANDO JUNGUNI
2.SHULE YA MSINGI NA KATI MABATINI
3.SHULE YA MSINGI MKOTE
4.SHULE YA SEKONDARI YA UKUNJWI
5.SHULE YA SEKONDARI FUNDO
6.SHULE YA MSINGI BOPWE
7.SHULE YA SEKONDARI YA KIZIMBANI
Mafanikio ya shule hizi ni ndogo, kila mwaka katika kupasisha wanafunzi matokeo ya kidato cha nne hua ni mabaya kwa asilimia 95%, kuna changa moto mbali mbali zinazosababisha ku feli kwa wanafunzi kiasi hicho, kwa utafiti uliofanywa na mwenyekiti wa kamati hii ya maendeleo ya Gando SALIM MUSSA OMAR, akishirikiana na waalimu, wanafunzi waliopo na waliomaliza akiwa na yeye ni mmoja wapo wa wahitimu wa shule moja wapo ya Gando, pamoja na wanakijiji waligundua kua miaongoni mwa sababu kuu ni kama ifuatavyo;
1.UKOSEFU WA MAABARA KATIKA SHULE ZOTE ZILIZOTAJWA.
2. MUINGILIANO WA WANAJAMII NA WANAFUNZI KWA MUDA ULIO MWINGI ZAIDI
KULIKO MUDA WA KUSOMA KWA MASHIRIKIANO YA WANAFUNZI KWENYE
MAZINGIRA YA KIUWANAFUZI, YAANI DAHALIA (BOARDING).
3. MUAMKO MDOGO KWA WANAFUNZI NA HATA WANA JAMII PIA.
4. UKOSEFU WA UFATILIAJI NA KUWEKA NGUVU KATIKA KUKAGUA UTENDAJI WA
WAALIMU NA MASHIRIKIANO YA WANAFUNZI KWA WAALIMU.
Hizi ni miongoni mwa sababu kuu zinazopelekea kufeli kwa kiwango kikubwa cha wanafunzi hawa wa Jimbo la Gando, Hivyo basi kama jumuia mpya ya kimaendeleo ya elimu na kijamii ya Gando imeona ni vyema kutafuta namna ya kupata wafadhili na misaada mbali mbali ili kuondoa hali hii haraka iwezekanavyo, kama kupatiwa dahalia (boarding schools) pamoja na kufanyika kwa safari za wanafunzi kutembelea sehemu mbali mbali ili kupata muamko wa kiwivu endapo wataona mafanikio ya wenziwao na kuzingatia kila kitu kinawezekana,
Baada ya kuona hali ni mbaya sana kwa Jimbo la Gando bila kua na muombezi uzalendo ulichukua na fasi na kuamua kuanzisha Gando development Foundation Kwa ajili ya kusaidia kuwango cha Elimu katika Mji wa Gando ili kusaidia kizazi Kipya na hata waalimu na wana jamii pia katika kushajihisha Maendeleo ndani ya jamii hii ilio tawaliwa na Umasikini wa kila namna, Gando Development Foundation Imeanzshwa tarehe 1/7/2012, chini ya mwenye kiti Salim Omar, akishirikiana kwa karibu sana na wanafunzi wenzake, na waalimu wake walioko chuo kikuu wanaotokea Gando na hata wanaotokea sehem nyengine katika kutafakari nini zuri lakuanza, hatima yake Gando Development foundation ime anza kutoa huduma ya Tenknolojia (ICT) katika shule za Gando, lengo ni kukuza na kuanzisha madarasa ya komputa kwa ajili ya muamko wa wanafunzi ili kushajihishika na pia kuzingatia mabadiliko na mapinduzi ya teknologia kila siku ziendapo mbele.
Kila kitu kinakua kinaanza kutambaa na nina imani foundation hii itakua ni chachu ya maendeleo ya Gando na hata sehemu nyengine pia za Pemba na Nje ya Pemba, kasoro za mradi huu ndo matengenezo ya baadae, tumeanza kutoa msaada wa komputa kumi kwa kila shule kati ya shule 6 zilizo tajwa hapo juu, tumeanza na shule ya Sekondari ya Gando, tunakaribisha mpenda maendeleo wowote katika kusaidia muendelezo wa mradi huu wa kusaidia Elimu kwa kizazi Kipya,
tembelea sehemu ya Mawasiliano na utapata kuwasiliana na wamiliki ama wakurugenzi wa mradi huu wa maendeleo, na wapenda maendeleo kama;
BWANA. SALIM MUSSA OMAR
MH. SAID ALI MBAROUK
BWANA. SAID KHAMIS FAKI
BWANA .SALIM ABDURRAHMAAN SEBIE
BWANA. SLIM KHALFAN SLIM
BWANA. DAVID NGURE NYAGA
BIBI . TUWAFU ALI ISSA
BIBI . SAUMU SAID
BWANA. SEIF FADHIL SERENGE
BWANA. SULEIMAN NASSOR SLEYUM
BWANA .ABDURRAHMA ALI NUHU
BWANA. AHMED ALI ABDULLAH
BWANA ABDULLAH OMAR HAMAD
No comments:
Post a Comment