JOGOO LIMEWIKA

Monday, October 8, 2012

JUHUDI ZA KIZALENDO KATIKA KUSUKUMA GURUDUMU LA MAENDELEO KATIKA KIJIJI CHA GANDO WETE PEMBA

  Malighafi kama mdalasini unaweza kusaidia kupungunza umasikini katika kijiji chetu cha Gando na ile dhana ya vijana walio wengi kutegemea tu ajira itapungua siku hadi siku, hivo basi tunawaomba wadau kutoka sehemu mbali mbali kusaidia ushauri na uwezo wa kuwawezesha wakaazi wa mji huu Wa Gando Wete Pemba kuweza ku export mali ghafi zao ili kupambana na janga la umaskini kwa wakaazi.
Huduma ya mawasiliano ni nyenzo moja wapo ya muhimu sana katika kurahisisha njia za maendeleo katika kijiji cha Gando Wete pemba, ukosefu wa mawasiliano ni moja ya kizingiti kikubwa kilichokuwepo dhidi ya mwanga wa maendeleo katika Mji wa Kijiji cha gando, tunashkuru juhudi za kujengwa kwa nyenzo hii ya mawasiliano, tuna ahidi kukanyaga ngazi hii kwa njia zilizo sahihi ili kuleta muamko wa maendeleo katika kijijji hichi kilicho jaa malighafi kama Mwani, mdalasini,asali,pilipili manga,karafuu, bizari,iliki,Mihogo, udongo wenye Rutuba kwa kuzalisha mazao tofauti tofauti, na uwepesishaji wa kufikisha teknologia ya masomo pia kwa kuanzishwa kwa madarasa ya komputa na intaneti.

No comments:

Post a Comment